Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Ugiriki lazima iheshimu masharti ya makubaliano ya kuinusuru nchi hiyo isifilisike kwa madeni yenye kuitaka serikali ya nchi hiyo kubana sana matumizi ya serikali ili iweze kupatiwa zaidi msaada wa kifedha.Mvutano juu ya mpango wa kima kikubwa cha fedha cha kuinusuru Ugiriki unatazamiwa kuugubika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya leo hii mjini Brussels huku kukiwa na hofu kuwa nchi hiyo inaweza kutoka kwenye kanda inayotumia sarafu ya euro barani Ulaya .Merkel amesema atakutana na baadhi ya viongozi pembezoni mwa mkutano huo akiwemo Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Rais wa Benki Kuu ya Ulaya Mario Draghi na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean Claude-Juncker.Kansela Merkel ameliambia bunge la Ujerumani kwamba ni jambo linalofahamika vyema kwamba hakuna mtu anayeweza kutarajia kupatikana kwa ufumbuzi wa matatizo ya Ugiriki usiku wa leo mjini Brussels au Jumatatu wakati Tsipras atakapofanya ziara yake ya kwanza mjini Berlin.
19 Machi 2015 - 19:24
Msimbo wa Habari: 677890
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Ugiriki lazima iheshimu masharti ya makubaliano ya kuinusuru nchi hiyo isifilisike kwa madeni yenye kuitaka serikali ya nchi hiyo kubana sana matumizi ya serikali ili iweze kupatiwa zaidi msaada wa kifedha